|
Mimi ni mtayarishaji wa muziki na mhandisi wa sauti toka Ufini. Umri wangu ni miaka 36. Nimeshawahi kufanya kazi miaka mingi kwenye medani za muziki, filamu, michezo ya kuigiza na dansi, aghalabu nchini Ufini na Tanzania.
Elimu ya msingi na secondary niliitimu Lohja, chuo cha sanaa (Torkkelin kuvataidelukio) nilisomea Helsinki, na shahada ya uzamili (MA) nilipata Theatre Academy of Finland, Dept. of Light and Sound Design.
Kwa maelekezo ya undani zaidi tafadhali pakua CV yangu katika umbizo ya PDF.
|